Unapojiandaa kuoa au kuolewa na unatarajia kufanya sherehe au hata usipofanya ukabariki tu yapo mambo yakuzingatia,hebu twende pamoja katika hili.....
Kuna vitu mnatakiwa kufanya kwa pamoja wawili mkishirikiana hata kama kuna mtu mwingine hapo anakuwepo kushauri na vyovyote vile katika kutoa mchango wake wa mawazo au pesa lakini wawili ni vizuri mkae pamoja mkubaliane baadhi ya vitu vya msingi...,
Ndoa nyingi zimekua na mambo ya kulaumiana baada ya sherehe kwisha kati ya ndugu au nyinyi wenyewe wawili.ili yasitokee hayo nimeamua kushare nanyi vitu vichache hivi hapa katika Blog ya My wedding Fashions.
Kaa na mwenzi wako mpange na kukubaliana rangi ya harusi.
Mavazi iwe full suit au koti juu rangi nyingine na suruali rangi nyingine.
Tai iwe neck tai,ndefu mpaka kwa magoti au ya aina gani ni we vile unapenda.
Sherehe iwe ya namna gani kwa ukumbi,iwe garden,nyumbani au kanisani,beach,sehemu ya wazi uwanjani kwa meli ndege au angani au makaburini ni nyie wawili kukubaliana ingawa na uwezo wa mtu unachangia au nafasi ya sehemu hizo zingine huwa zinakua booked for a long time.
PICHA NA VIDEO(Still Picture&Video)
Mtu wa kupiga picha za mnato na video hapa ndo kasheshe ukikosea hapa umefuta kumbukumbu zote na ukiharibu hapa hata picha utakua huna hamu nazo kuziangalia mara kwa mara,zitakuchosha haraka sana.
Tafuteni mpiga picha mzuri ambae atapiga picha zenu mtazipenda awe anafahamu matukio muhimu na ndugu za pande mbili anakumbuka kupiga picha sio ilimradi picha tu. unakosa hata kumbukumbu na picha za wazazi pamoja na maharusi wadogo zako au kaka zako rafiki wale wa karibu inaboa sana kwakweli,kumbukumbu ni jambo la muhimu sana katika matukio kama haya ni mara chache sana kutokea na sometimes likitokea mara moja ndo basi tena sa usikubali mtu akuharibie picha zako.Siku hizi technologia imekua watu wanaweka picha nyingi sana ambazo we mwenyewe unaweza chagua au akatoa zote mshiko wako tu na hata album ikipotea zikichanika dogo akizimwagia maji unaweza ukazipata tena kwa kuhifadhi katika flash,cd computer yako. achana na mtu asie na storage ya kutosha kuhifadhi kumbukumbu yako hatoi cd, hana flash au basi aseme nipe flash nikuwekee nyingine humo,
video ni hayohayo tu zipo video productions unapenda uangalie harusi yako daily inapendeza matukio muhimu yote yapo tena kitu clearrrrrrrrrrr.....digital (sio analogia mchelemchele rekebisha antena) hayo mambo yashapitwa na wakati tafuta video productions za ukweli zipendezeshe you day.
PETE/RING
Pete ndo mpango mzima katika jambo hili mchungaji/padri/shekhe,hakimu,chief au yeyote yule anaefungisha ndoa,atakuuliza umekuja na pete? Pete bana ndio pale unaonyesha jinsi gani upo serious na jambo hilo unaonyesha kwamba unampenda huyo binti.
Inapendeza mkienda wote kuchagua aina ya pete mngependa kuvaa siku ya harusi yenu iwe gold,silver,copper au ya udongo ni nyie wawili ndio mnapaswa kuamua hii pia inategemea na uwezo wenu hasa bwana harusi. sio unamlazimisha mwenzio anunue pete za milion mbili wakati uwezo wa mwenzako laki mbili acha mambo hayo......
SALOON
Hapa sasa mmhhh..!!!
Saloon ni sehemu ambayo mtu anaenda kufanya urembo au kupasha misuli na mambo mengine mengi tu yanayohusiana na urembo.
Bi Harusi aiseee aende saloon amezoea kurembwa kama anaenda kwa mgeni basi huyo mgeni awe mkali kwelikweli kwa mambo ya urembo mana dah.., mtu anaweza kununa harusi nzima mwanzo mwisho acheki kisa wamemzingua usoni. Acha kabisa sura siku hiyo ndio mambo yote ukiharibu kwa sura hata mpiga picha nahisi anaweza nae kuchemsha poda imezidi make up wamemkosea upande huu nyingi huku hamna,zile nyusi bora asingenyoa,ile shedo sasa mmhh!!! hivyo ni vijimambo ambavyo wageni waalikwa wifiz teh (wifi) wataongea acha tu, na muhusika akigundua wamemuharibu usoni na muda ndo umefika anatakiwa aondoke aende akafunge ndoa kazi kwelikweli. kulia anataka kununa anataka hasira kibao hapo mambo hayaendi kabisa ni bora haya mambo yakaandaliwa mapema kabisa.
Ndugu zako wamenilazimisha niende ile saloon mi nlitaka kwenda ya kwetu tabata we umenipeleka sinza ona walivyoniharibu sasa...
Lawama kama hizo zaweza kuepukwa pale mnapokubaliana kwa moyo moja kwamba uende saloon fulani linakua ni jambo zuri.
Zipo saloon za ukweli ambazo hata ukienda una milima ya namna gani usoni na mabonde mambo yako yanaenda sawa zipo zipo sikatai ila maandalizi mapema ni muhimu ili siku yako isiharibike kwa kununa siku nzima,fanya siku yako uwe na amani kwa kupendeza.
Endelea kufuatilia ushauri wa bure katika Blog yetu Myweddingfashions kwa mambo mazuri zaidi kwa leo let me end here see you next time(kidhungu hapo)
No comments:
Post a Comment