Sunday, December 23, 2012

WELCOME

Welcome to the Blog,My wedding Fashions.

I would like to take this opportunity to thank God, for his great goodness to give me Health,Life,Power and a Sound Mind in making my Idea successful. I would also like to say thanks to my beloved Wife, Friends,and Relatives for taking their time to advice,encourage and to make my dream possible under the sun.

This Blog is a continuation of an Idea /concept of the original Idea of having a wedding Magazine,but because of the challenges we faced on the process,we have decided to begin with Blog spot and the Magazine will follow later,,,,,......

This Blog is for all people of goodwill in Tanzania,Africa and the whole world.The Blog is used to teach,advice,encourage,inform and connect you with different  business and service provider for your festival,wedding ceremony,kitchen and send off party.
The Blog is also dealing with educating young people about marriage before and after marriage,relationships,sexual and reproductive health,Family Planning and counselling on HIV/AIDS.
The Blog is giving you the right information on how to contact the Mc's Music,Video Productions,Still Pictures,Conference Hall,Ceremony Organizer,cake practitioners,decorations,Vehicles, Jewellery's,Food Services,Suit and Gowns for bride and bloom,shoes and Hotels for your Honeymoon.

The Informations are available to make your day be memorable and happy day ...............
You may contact us through E mail,Facebook,Twitter,Blog Mobile Phones shows on the Blog. 
Thank you for your time visiting our Blog....
TO GOD BE THE GLORY.




Mr&Mrs Robert Mwamakamba


Mr Robert Mwamakamba


Sally Picture on Her Wedding Day


CAKE

Mbali na bibi harusi kupendea siku yake ya harusi kuna jambo lingine muhimu likawepo siku hiyo.......
Kabla ya kwenda kuonana na anaekuandalia cake ya harusi yako kuna mambo muhimu kuzingatia;
unaweza tazama aina ya cake mbalimbali kupitia internet,vitabu vya mapishi ,marafiki,mtandao na sherehe mbalimbali uliowahi kupitia kwa ajili ya reference/ili ufanyapo uchaguzi uwe bora.

LADHA /Flavours and Texture
  • Hakuna haja ya kuwa na cake nzuri imepambwa vizuri halafu ishindwe kuliwa na wageni waalikwa pamoja na maharusi, cake inatakiwa kuwa nzuri/tamu nje na ndani, ongea/shauriana  na muandaaji wa cake yako kuhusu ladha na muonekano wa cake yako kuna ladha mbalimbali za kuchagua ni vile unapenda iweje kutegemea na rangi mliochagua ya harusi yenu au vile nyie mnapenda kama; carrot,fruitcake,vannila,chocolate,strawberry,coconut,lemon,banana,orange,red velt, kwa hizo chache...
  • uchaguzi ni wako ipi iwepo kwa sherehe yako au zipi ziwepo kwa sherehe yako 
SHAPE AND SIZE
  • Unaweza kuchagua size mbalimbali na aina gani ya shape unapenda iwe kutokana na wajuzi wengi wa mambo haya sikuhizi unaweza tengenezewa size na shape yeyote ile we unapenda.
  • Ukiwa na design yako pia ni nzuri unamuonyesha tu anaendaa cake yako 

PRESERVING THE CAKE/UTUNZAJI WA CAKE
  • Baada ya harusi cake nyingi zinaaribika kwa kutokutunza vizuri
  • Weka kwa chombo kinachopitisha hewa vizuri
  • Usizungushe na foil
  • Weka mbali na vitu kama vitunguu......
  • Tumia fridge au hata mezani sehemu safi funika na kitu kizuri.
Leo ni Hizo Tips chache ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

CAKE FOR YOUR WEDDING
 Apart from the Bride to Love her wedding day,there is another important things to consider for your day.
before you meet to the one who will prepare your wedding cake,it is important to search for variety of cakes via internet,recipe books,friends ,Networking and various ceremonies for reference.

TASTE ,FLAVOUR &TEXTURE
There is no need to have a beautiful cake,that cannot be eaten by invited guest. cake should be sweet.
Talk to your practitioner on appropriate design of your cake,about the taste,appearance and delicious range of choice is depending on how you want.
This may also depend on the chosen colour of your wedding,here are some of the flavors of the cakes you may like fruit cake,vanilla,chocolate,strawberry,coconut,lemon banana,orange,and redvelt. Its you to decide what are your choices exist for your ceremony,or what to have for your party.

SHAPE&SIZE
There is different size and shape,you can choose what kind of shape you want to be in your wedding because many of these practitioners can make any size and shape you want.
If you prefer to design by yourself its good you tell them before they make it.

PRESERVATION
After wedding many cakes becomes useless cannot be eaten anymore,I advice to preserve the cake carefully.
Keep the container properly where an air can get through
Keep away from things like onions and moisture
Keep on dry surface
Keep it open like on the table but don't put it for a long time to avoid dust
Use fridge to preserve.


Friday, December 14, 2012

Budget for the Wedding

Budget is a financial  plan/Budget for something like wedding or a party is amount of money that a person,organisation,or a country has available to spend.
Its very important to have a money plan towards your wedding,It shows a way on how your going to spend,this is either you do from your pocket or you get support from your friends,relatives and parents. It is a must to have Budget.
Budget will make you easy to understand how many guests you expect to attend in your wedding.
It helps to know exactly what to have in the wedding party and how much will it cost.
It helps to know how many friends,and relatives that can contribute to your wedding and this also will make easy for you to understand the way of collecting cash from them.

Note:
A bride and Groom should have their own budget separate from what am talking about.
Special People like bride and groom there some items that should be included in their budget Suit,bride gown,shoes,rings,shirts,vest,belt,socks,boxer,pocket money,etc.
Parents have to consider to buy a bag for their child (BOY) you know what to put in,,,,there.., for honeymoon to be fantastic..(sio asubuhi aanze kutafuta mswaki uko wapi??)

Words of Encouragements/

Do you long for peace and happiness?
Dont  look around,look within yourself.
Everything you need lies within your own heart;
choose to listen to your soul, and follow your inner guidance for direction.

Sunday, December 9, 2012

Ushauri wa Bure

Unapojiandaa kuoa au kuolewa na unatarajia kufanya sherehe au hata usipofanya ukabariki tu yapo mambo yakuzingatia,hebu twende pamoja katika hili.....
Kuna vitu mnatakiwa kufanya kwa pamoja wawili mkishirikiana hata kama kuna mtu mwingine hapo anakuwepo kushauri na vyovyote vile katika kutoa mchango wake wa mawazo au pesa lakini wawili ni vizuri mkae pamoja mkubaliane baadhi ya vitu vya msingi...,

Ndoa nyingi zimekua na mambo ya kulaumiana baada ya sherehe kwisha kati ya ndugu au nyinyi wenyewe wawili.ili yasitokee hayo nimeamua kushare nanyi vitu vichache hivi hapa katika Blog ya My wedding Fashions.

Kaa na mwenzi wako mpange na kukubaliana  rangi ya harusi.
Mavazi iwe full suit au koti juu rangi nyingine na suruali rangi nyingine.
Tai iwe neck tai,ndefu mpaka kwa magoti au ya aina gani ni we vile unapenda.
Sherehe iwe ya namna gani kwa ukumbi,iwe garden,nyumbani au kanisani,beach,sehemu ya wazi uwanjani kwa meli ndege au angani au makaburini ni nyie wawili kukubaliana ingawa na uwezo wa mtu unachangia au nafasi ya sehemu hizo zingine huwa zinakua booked for a long time.

PICHA NA VIDEO(Still Picture&Video)
Mtu wa kupiga picha za mnato na video hapa ndo kasheshe ukikosea hapa umefuta kumbukumbu zote na ukiharibu hapa hata picha utakua huna hamu nazo kuziangalia mara kwa mara,zitakuchosha haraka sana.
Tafuteni mpiga picha mzuri ambae atapiga picha zenu mtazipenda awe anafahamu matukio muhimu na ndugu za pande mbili anakumbuka kupiga picha sio ilimradi picha tu. unakosa hata kumbukumbu na picha za wazazi pamoja na maharusi wadogo zako au kaka zako rafiki wale wa karibu inaboa sana kwakweli,kumbukumbu ni jambo la muhimu sana katika matukio kama haya ni mara chache sana kutokea na sometimes likitokea mara moja ndo basi tena sa usikubali mtu akuharibie picha zako.Siku hizi technologia imekua watu wanaweka picha nyingi sana ambazo we mwenyewe unaweza chagua au akatoa zote mshiko wako tu na hata album ikipotea zikichanika dogo akizimwagia maji unaweza ukazipata tena kwa kuhifadhi katika flash,cd computer yako. achana na mtu asie na storage ya kutosha kuhifadhi kumbukumbu yako hatoi cd, hana flash au basi aseme nipe flash nikuwekee nyingine humo,
video ni hayohayo tu zipo video productions unapenda uangalie harusi yako daily inapendeza matukio muhimu yote yapo tena kitu clearrrrrrrrrrr.....digital (sio analogia mchelemchele rekebisha antena) hayo mambo yashapitwa na wakati tafuta video productions za ukweli zipendezeshe you day.

PETE/RING
Pete ndo mpango mzima katika jambo hili mchungaji/padri/shekhe,hakimu,chief au yeyote yule anaefungisha ndoa,atakuuliza umekuja na pete? Pete bana ndio pale unaonyesha jinsi gani upo serious na jambo hilo unaonyesha kwamba unampenda huyo binti.
Inapendeza mkienda wote kuchagua aina ya pete mngependa kuvaa siku ya harusi yenu iwe gold,silver,copper au ya udongo ni nyie wawili ndio mnapaswa kuamua hii pia inategemea na uwezo wenu hasa bwana harusi. sio unamlazimisha mwenzio anunue pete za milion mbili wakati uwezo wa mwenzako laki mbili acha mambo hayo......

SALOON
Hapa sasa mmhhh..!!!
Saloon ni sehemu ambayo mtu anaenda kufanya urembo au kupasha misuli na mambo mengine mengi tu yanayohusiana na urembo.
Bi Harusi aiseee aende saloon amezoea kurembwa kama anaenda kwa mgeni basi huyo mgeni awe mkali kwelikweli kwa mambo ya urembo mana dah.., mtu anaweza kununa harusi nzima mwanzo mwisho acheki kisa wamemzingua usoni. Acha kabisa sura siku hiyo ndio mambo yote ukiharibu kwa sura hata mpiga picha nahisi anaweza nae kuchemsha poda imezidi make up wamemkosea upande huu nyingi huku hamna,zile nyusi bora asingenyoa,ile shedo sasa mmhh!!! hivyo ni vijimambo ambavyo wageni waalikwa wifiz teh (wifi) wataongea acha tu, na muhusika akigundua wamemuharibu usoni na muda ndo umefika anatakiwa aondoke aende akafunge ndoa kazi kwelikweli. kulia anataka kununa anataka hasira kibao hapo mambo hayaendi kabisa ni bora haya mambo yakaandaliwa mapema kabisa.
Ndugu zako wamenilazimisha niende ile saloon mi nlitaka kwenda ya kwetu tabata we umenipeleka sinza ona walivyoniharibu sasa...
Lawama kama hizo zaweza kuepukwa pale mnapokubaliana kwa moyo moja kwamba uende saloon fulani linakua ni jambo zuri.
Zipo saloon za ukweli ambazo hata ukienda una milima ya namna gani usoni na mabonde mambo yako yanaenda sawa zipo zipo sikatai ila maandalizi mapema ni muhimu ili siku yako isiharibike kwa kununa siku nzima,fanya siku yako uwe na amani kwa kupendeza.

Endelea kufuatilia ushauri wa bure katika Blog yetu Myweddingfashions kwa mambo mazuri zaidi kwa leo let me end here see you next time(kidhungu hapo)




Monday, December 3, 2012

KARIBU WELCOME


Karibu katika blog hii.........Myweddingfashion


Napenda Kuchukua Fursa hii, kumshukuru Mungu, kwa wema wake mkuu kunipa Afya,Uzima,nguvu na Akili timamu katika kufanikisha idea yangu hii, pili  Mke wangu mpenzi, Rafiki zangu kuniwezesh katika ushauri kunitia moyo na kuniaminisha kuwa hakuna lisilowezekana chini ya jua.

 Blog hii....... ni mwendelezo wa idea/wazo la awali kuwa na gaeti linalohusu mambo ya harusi sendoff kitchen party zikiambatana na picha za matukio ya sherehe hizo. kutokana na mambo kwenda ndivyo sivyo tukaaamua kuwa na blogspot kwanza na gazeti litafuata baadae............
Blog hii ni kwa watu wote wenye nia njema Tz,Africa na Ulimwengu wote.
Blog inapenda kukuhabarisha mambo mbalimbali yanayohusu sherehe ya harusi kabla na baada ya harusi.........

Blog ipo kukusaidia katika kupata maelezo/information ya vitu muhimu kwa sherehe ya harusi yako/sendoff party na kitchen party.

Kupitia blog hii utapata kuwa na MC'z wazuri kwa sherehe yako waandaaji wa Cake, Ukumbi,Wapambaji, Magari, Video na Still Picture.

Blog hii inatumia lugha zote za mawasiliano katika kufanikisha makusudio yake Kiswahili lugha kuu,English French German etc

Wasiliana nasi kupitia namba za simu hizo hapo juu ,E mail facebook,twitter nasi tutakujuza ukitakacho.
Karibu katika Myweddingblogspot.com.............................!!

Thanks.......................